Home Uncategorized BAADA YA SVEN KUONYESHA KUMUHITAJI..KIUNGO NAMUNGO AMEFUNGUKA HAYA..!!

BAADA YA SVEN KUONYESHA KUMUHITAJI..KIUNGO NAMUNGO AMEFUNGUKA HAYA..!!

KOCHA wa Simba, Mbelgiji Sven, hakuficha hisia zake namna anavyomkubali kiungo wa Namungo FC, Lucas Kikoti ‘Mtakatifu Kikoti’, sasa mchezaji mwenyewe amesisitiza, ikitokea Wekundu hao wa Msimbazi wanamuhitaji, hatajiuliza mara mbili.

Kikoti alisema hakuna asiyejua Simba ni miongoni mwa timu kubwa na nzuri na sehemu kubwa ya wachezaji wanatamani kucheza haoo.

“Ikitokea kama Simba wananihitaji, yaani fasta nitakuwa tayari kwenda huko hata sitajiuliza mara mbili. Unajua mPira ni kazi yangu hivyo natakiwa kuPambana. Jambo la muhimu kumalizana na mabosi wangu wa Namungo,” alisema Kikoti ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha Taifa Stars.

Hii inaweza kuwa mara ya kwanza kwa Sven kumtaja mchezaji anayemkubali wazi mbele ya kadamnasi.

“Siwajui kwa majina wachezaji wengi ila nawatambua kwa namba. Yule anavaa namba nane Namungo anacheza kiungo mshambuliaji (kikoti) namfatilia. Ni mchezaji mzuri, naoenda anavyocheza. Anacheza kwa nafasi akifuata maelekezo, alifunga bao zuri dhidi yetu, anajua anachofanya, ametulia na yuko smati,” alisema Sven kocha ambaye amekuwa akifanya mambo yake kimya kimya.

Kikoti alikwenda mbali na kufunguka mkataba wake na furaha hiyo.

“Na nimefurahi kuona kumbe hâta makocha wakubwa kama huyo wa Simba anatambua uwezo wangu, najifunza kuwa natakiwa kuongeza juhudi zaidi ili nifanikiwe.

“Mkataba wangu na Namungo upo hadi mwakani, lakini tuna makubaliano maalumu, jambo linalonioa urahisi wa kwenda timu yoyote husika.”

    

SOMA NA HII  MMOJA TEGEMEO YANGA ANASWA AZAM