Home Uncategorized BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS

BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS


JUVENTUS imethibitisha kuachana na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Maurizio Sarri baada ya kudumu kwa msimu mmoja ndani ya klabu hiyo.

Sarri aliibukia ndani ya Juventus akitokea Chelsea ambapo ndani ya msimu wa 2019/20 alifanikiwa kutwaa taji la Serie A ila kuchemka kwa timu yake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kuishia hatua ya 16 bora kumemponza.

Kocha huyo mwenye miaka 61 licha ya uwezo wake mkubwa wa kufundisha bado hajawakosha mabosi wake wa Juventus jambo lililomfanya wamtimue mazima.

Kupoteza mbele ya Lyon mchezo wa usiku wa kuamkia leo kumewakasasirisha mabosi wa Juventus na kuamua kumfungashia virago. 

Mchezo wake wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Lyon alishinda kwa mabao 2-1 ila haikumpa nafasi ya kusonga mbele kwa kuwa mchezo wa kwanza alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kabla ya janga la Corona kuvuruga masuala ya ratiba zote duniani.


Hivyo Lyon ilisonga mbele hatua ya nusu fainali kwa faida ya bao la ugenini.

SOMA NA HII  HIKI NDICHO KILICHOMPONZA CHIRWA, SINGANO, LYANGA KUPIGWA CHINI AZAM FC