Home Uncategorized BREAKING:AZAM FC YAMALIZANA NA MAKOCHA WATATU

BREAKING:AZAM FC YAMALIZANA NA MAKOCHA WATATU

 


UONGOZI wa Azam FC, leo Agosti 25 umemalizana na makocha wake watatu wanaounda benchi la ufundi kwa ajili ya kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.

Makocha hao ambao wameongeza  mkataba leo ni pamoja na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, raia wa Romania.

 Kocha Msaidizi, Bahati Vivier na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, ambapo kila mmoja ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Agosti 23, Azam FC waliwatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi ambalo lilianza kazi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namung FC.

Kwenye mchezo huo uliohudhiuriwa na mashabiki wengi, Azam FC ilishinda mabao 2-1, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA:HARUNA NIYONZIMA HANA NIDHAMU