Home Uncategorized CHAMA AKUBALI MUZIKI WA TIMU YAKE YA SIMBA

CHAMA AKUBALI MUZIKI WA TIMU YAKE YA SIMBA

 

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, amefunguka kuwa kutokana na ubora wa kikosi chao kwa sasa, ana imani kuwa hakuna timu yoyote itakayoweza kupona katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwani imetimia katika kila idara.

 

Chama ametoa kauli hiyo kufuatia Jumamosi iliyopita, Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’O ya Burundi katika mchezo wa tamasha la Simba Day uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

 Chama alisema kuwa anaamini Simba ya sasa imekuwa ya moto na haitaweza kuzuiwa na timu yoyote kutokana na kukamilika kwa kila idara baada ya uongozi kufanya usajili mkubwa.

 

“Kikubwa kwamba timu imekuwa na mabadiliko makubwa kwa sababu ukubwa wa mashindano ambayo yapo mbele yetu na kila mtu ameona timu ilivyokuwa bora na yenye ari ya kutaka mataji.

 

“Naamini hii itasaidia kushinda kila mchezo ambao upo mbele yetu kuanzia kwenye ligi ambayo tunahitaji kutetea ubingwa kwa mara nyingine lakini katika michuano ya kimataifa hasa ukizingatia ubora ambao kila mchezaji anao na hilo ndiyo lengo kubwa kwa msimu huu,” alisema Chama.


Chanzo:Championi

SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING