Home Habari za michezo HUU HAPA UFAFANUZI WA AHADI YA RAIS SAMIA KWA SIMBA NA YANGA…KILA...

HUU HAPA UFAFANUZI WA AHADI YA RAIS SAMIA KWA SIMBA NA YANGA…KILA MCHEZAJI KUVUNA MAMIIONI…

Habari za Micheo

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ametangaza kulinunua kwa Tsh. Milioni 5 kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga katika michezo yao inayochezwa weekend hii wakiiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Shirikisho.

Taarifa hiyo imetolewa kwa Wahariri na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Dar es salaam ambapo amenukuliwa akisema “Rais Samia amenituma nisemae kila goli litakalofungwa na Yanga au Simba ametangaza kulinunua kwa Tsh. Milioni 5”

“Kazi kwenu Wachezaji ukifunga magoli mawili una Tsh. Milioni 10, ukifunga magoli matano una Tsh Milioni 50, lengo lake pamoja na kufunga magoli Timu zetu lazima zishinde kwenye michuano hii”

Simba SC ni Wawakilishi wa Tanzania katika michuno ya Club Bingwa Afrika na watacheza dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco Jumamosi hii uwanja wa Mkapa wakihitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika Kundi wakati Yanga SC wenyewe wanacheza Jumapili kwa Mkapa dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wote wanahitaji ushindi ili kumaliza nafasi mbili za juu na baadae kukata tiketi ya robo fainali.

SOMA NA HII  IANZE WIKI YAKO KWA KUSHINDA MTINYO KIULAIINI KUPITIA CASINO YA KENO NDANI YA MERIDIABET..