Home news COASTAL UNION: BADO TUPO KWENYE MAPAMBANO

COASTAL UNION: BADO TUPO KWENYE MAPAMBANO


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa bado mashindano yanaendelea hivyo watapambana kwa mechi ambazo zimebaki kupata matokeo chanya.

Kwenye msimamo Coastal Union ipo nafasi ya 17 imekusanya pointi 34 baada ya kucheza mechi 32.

Mchezo wake uliopita ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Coastal Union na kufanya timu hiyo kuyeyusha pointi tatu mazima mbele ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Mgunda amesema kuwa bado mashindano yanaendelea wanaamini watafanya vizuri.

“Tumepoteza mbele ya Simba sawa nakubali kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi na kwa ambacho kimetokea kila mtu anakiona.

“Bado tupo kwenye mashindano na kila timu inahitaji ushindi hivyo tutapambana kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo zimebaki,” amesema.

 

SOMA NA HII  BAADA YA UJIO WA SURE BOY...MUKOKO AKATAA MKATABA MPYA YANGA...SIMBA WAHUSISHWA....