Home news ILE ISHU YA USAJILI WA MNIGERIA ETOP DAVID UDOH KUJIUNGA SIMBA IKO...

ILE ISHU YA USAJILI WA MNIGERIA ETOP DAVID UDOH KUJIUNGA SIMBA IKO HIVI…KUMBE NAYE NI WALEWALE TU….


Kiungo Kutoka nchini Nigeria aliyetawala kwenye Mitandao ya Kijamii wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Simba SC dhidi ya Selem View Etop David Udoh huenda akaonekana kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha klabu hiyo kesho Ijumaa (Januari 07) dhidi ya Mlandege FC.

Simba SC ilianza kusaka ubingwa wa Mapinduzi 2022 jana Jumatano (Januari 05), kwa kucheza dhidi ya Selem View na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, yaliyofungwa na Pape Ousman Sakho na Rally Bwalya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, anatarajiwa kucheza mchezo wa kesho kama sehemu ya majaribio, na kama atamridhisha Kocha Mkuu Franco Pablo Martin, atasajiliwa katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Kabla ya kuja Tanzania, Udoh alikuwa akikipiga katika klabu ya Arar FC ya Saudi Arabia inayoshiriki ligi dalaja la pili.

Udoh anakuwa Mchezaji wa tatu kutua Simba SC kufanya Majaribio baada ya Sharaf Shiboub raia wa Sudan na Moukoro Cheikh Tenera raia wa Ivory Coast ambao wote jana walicheza dhidi ya Selem View.

SOMA NA HII  MALIZIA MECHI ZA AFCON KWA MKWANJA MKUBWA KUTOKA MERIDIANBET...ODDS ZOTE HIZI HAPA..