Home Uncategorized MEDDIE KAGERE KUSEPA SIMBA MAZIMA

MEDDIE KAGERE KUSEPA SIMBA MAZIMA



INAELEZWA kuwa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck haziivi chungu kimoja jambo linalomfanya ajenge ushkaji na benchi.


Hali hiyo inatajwa kuwa sababu ya Kagere kuweza kusepa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hajui hatma yake itakuaje kwenye maisha yake ya kucheza ndani ya uwanja.


Kagere amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu ambapo inaelezwa kuwa alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma ila aliitwa kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda.


Kwa msimu huu wa 2020/21 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikiwa imecheza mechi mbili na kutumia dakika 180 uwanjani, nyota huyo ametumia dakika mbili pekee.


Wakati ikishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau Uwanja wa New Jos, Kagere aliishia benchi huku mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikiambulia sare ya bila kufungana aliingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya John Bocco na kutumia dakika mbili ndani ya uwanja.


Suala hilo linatajwa kuwa sababu ya chanzo cha nyota huyo kufungua njia ya kusepa ndani ya kikosi hicho ambacho amekifungia jumla ya mabao 49 ndani ya ligi.


Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wote wana uwezo mkubwa wa kucheza na kila mmoja ana umuhimu wake.

SOMA NA HII  KAMA UTANI VILE KOCHA NAMUNGO ABWAGA MANYANGA