Home Yanga SC NYOTA WATANO WA YANGA KUIKOSA MTIBWA SUGAR KWA MKAPA

NYOTA WATANO WA YANGA KUIKOSA MTIBWA SUGAR KWA MKAPA


IKIWA leo Yanga inayoongoza Ligi Kuu Bara inashuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar itakosa huduma za nyota wake watano.

Inashuka uwanjani ikiwa inakumbuka kwamba imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu FC.

Walipokutana mara ya kwanza Uwanja wa Jamhuri, Moro, Yanga ilisepa na pointi tatu mazima kwa ushindi wa bao 1-0 leo inakutana nao Uwanja wa Mkapa.

Hawa hapa nyota watano wa Yanga wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo:- Saido Ntibanzokiza, yeye anasumbuliwa na majeraha ya nyonga aliyapata kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kisha akajitonesha kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba, fainali visiwani Zanzibar.

Beki, Dickson Job majeraha ya nyama za paja yanamsumbua ila ameanza mazoezi mepesi kurejea kwenye ubora wake.

Yacouba Songne taratibu ameanza kurejea kwenye ubora wake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, dhidhi ya Azam FC.

Mapinduzi Balama, nyota huyu kwa sasa jezi yake namba 7 ipo mikononi mwa Fiston Abdoul Razack kwa kuwa anatibu majeraha yake ya mguu.

Ramadhan Kabwili, kipa namba tatu wa Yanga hayupo kwenye hesabu za Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

SOMA NA HII  HAYO MAANDALIZI YA GAMONDI DHIDI YA AL MAREIKH SIO POA