Home news BAADA YA UJIO WA SURE BOY…MUKOKO AKATAA MKATABA MPYA YANGA…SIMBA WAHUSISHWA….

BAADA YA UJIO WA SURE BOY…MUKOKO AKATAA MKATABA MPYA YANGA…SIMBA WAHUSISHWA….


HABARI si njema kwa mashabiki wa Yanga kutokana na kudaiwa kuwa kiungo mkabaji wa timu hiyo, Mukoko Tonombe kugomea mkataba mpya kikosini hapo.

Mukoko ndani ya Yanga amejikuta akipoteza nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza msimu huu kutokana na uwepo wa viungo Khalid Aucho na Yanick Bangala ambao wamesajiliwa msimu huu.

Wakati Mukoko akiwa hatihati kubaki Yanga, taarifa kutoka Simba zinadai kwamba, tayari uongozi wa klabu hiyo umeanza kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo ambaye mkataba wake umebaki miezi sita kabla ya kumalizika.

Kwa sasa Simba inasaka kiungo mkabaji mara baada ya Tadeo Lwanga kuwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Simba kwa sasa inatafuta kiungo mkabaji wa kuja kuchukua nafasi ya Tadeo Lwanga na tayari uongozi wa Simba unafahamu kuwa Mukoko Tonombe mkatabawake na Yanga umebaki miezi sita, hivyo lolote linaweza kutokea.

“Mukoko ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza kikosi cha timu yoyote katika ligi yetu, hivyo kuwa naye katika kikosi ni moja ya kuwa na silaha nzuri ya kivita ambayo muda wowote ipo tayari kwa mapambano,” kilisema chanzo hiko.

Naye rafiki wa karibu wa Mukoko Tonombe kutoka DR Congo ambaye hakutaka jina lake kutajwa, alisema:

“Mukoko Tonombe kwa sasa hana furaha ndani ya Yanga, sio kama ilivyokuwa hapo awali, hii inatokana na yeye kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara na hataki kuongoza mkataba akihitaji changamoto sehemu nyingine.

“Yeye mwenyewe alikuwa na malengo ya kuisaidia Yanga, lakini kwa sasa hali imebadilika na aliniambia kuwa AS Vita wanajaribu kumrudisha nyumbani, lakini kuna ofa amepokea kutoka timu kubwa kutoka Tanzania, hivyo ngoja tuone nini kitatokea.”

SOMA NA HII  ISHU YA AUCHO YASHUSHA PRESHA YANGA...SASA NI UHAKIKA ASILIMIA ZOTE JAMBO LIPO....