Home news RASMI…AJIB MALI YA AZAM FC…SIMBA WAVUNJA UKIMYA..WAANIKA SABABU ZA KUMTEMA….

RASMI…AJIB MALI YA AZAM FC…SIMBA WAVUNJA UKIMYA..WAANIKA SABABU ZA KUMTEMA….


UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha kusitisha mkataba wa kiungo fundi Ibrahim Ajibu ambaye amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba imeeleza kuwa imefikia makubaliano ya pande zote mbili kwa maslahi mapana kusitisha mkataba wa kiungo huyo mshambuliaji.

Ajibu alirejea nyumbani kwa mara nyingine tena akitokea Yanga ambapo alipokuwa huko alikuwa ni nahodha na alipofika Simba mambo yalikuwa magumu kwake.

Jana Desemba 29 wakati wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi Uwanja wa Bunju Complex kujiaandaa na mchezo ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Januari Mosi 2022 Uwanja wa Mkapa hakuwepo mazoezini.

SOMA NA HII  DILI LA OPUKU KUTUA SIMBA SC LAFIA KWENYE MAKARATASI...ISHU NZIMA IKO HIVI....