Home Uncategorized NCHIMBI ABADILI GIA YANGA

NCHIMBI ABADILI GIA YANGA


STRAIKA mpya wa Yanga, Ditram Nchimbi, amekuja na wazo jipya katika kuhakikisha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara anatoka ndani ya kikosi chao, hivyo yeye amejipa rasmi kazi ya kuwatengenezea wenzake mabao ili watwae Kiatu cha Dhahabu.

Katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Nchimbi alitoa pasi ya bao lililofungwa na mshambuliaji mwenzake, David Molinga, ambaye amefikisha idadi ya mabao sita mpaka sasa.

Nchimbi alisema nafasi hiyo ni muhimu kwake lakini kwa sasa yupo kwa ajili ya timu zaidi hivyo anatamani kuona anakuwa na mchango mkubwa katika kumtoa mfungaji ndani ya kikosi chake.

“Si rahisi kusema nafukuzia ufungaji bora, lakini ukiangalia wapo ambao wana mabao mengi na wenye nafasi hiyo zaidi yangu, ukweli mimi nitafurahi nikiona anakuwa sehemu ya mafanikio ya mchezaji wa timu yangu akipata nafasi hiyo,” alisema Nchimbi.

Nchimbi aliyetua Yanga akitokea Polisi Tanzania ameongeza kuwa amekuwa na wakati mzuri ndani ya timu kutokana na ushirikiano uliopo kati yake na wachezaji wenzake, sambamba na benchi la ufundi hali inayozidi kumfanya ajiamini zaidi.

Kwasasa nafasi hiyo hiyo bado inafukuziwa na straika wa Simba, Meddie Kagere, mwenye mabao 12 akifatiwa na Paul Nonga pamoja na Daruwesh Saliboko wote kutoka Lipuli kila mmoja akiwa na mabao nane.
SOMA NA HII  KOCHA WYDAD AWAANGALIA MASHABIKI WAO KISHA AKAWAPA HABARI HII.... HIKI NDICHO ITAKACHOAMBULIA SIMBA HUKO MARRAKESH