Home kimataifa ARSENAL KUMCHOMOA KIUNGO MADDISON NDANI YA LEICESTER CITY

ARSENAL KUMCHOMOA KIUNGO MADDISON NDANI YA LEICESTER CITY


ARSENAL imetoa ofa kwa Leicester City ya kutoa fedha pamoja na mchezaji kati ya Hector Bellerin ama Eddie Nketiah ili kumpata kiungo James Maddison.

Kwa sasa Arsenal imekuwa ikumuwinda nyota huyo ili aweze kujiunga na timu hyo kwa msimu ujao ndani ya Ligi Kuu England.

Thamani ya mchezaji huyo ni kiasi cha pauni milioni 60 na mabosi wake Leicester wameweka wazi kwamba huo ni mkwanja ambao wanahitaji.

Aliibuka ndani ya Leicester City akitokea Klabu ya Norwich mwaka 2018 kwa ada ya pauni milioni 25 hivyo thamani yake imepanda kutokana na uwezo wake.

Dau ambalo wametajiwa Arsenal inaonekana kabisa watashindwa kumudu jambo ambalo limewafanya waweze kutoa ofa ya mchezaji ili kuipata saini ya nyota huyo.

SOMA NA HII  KUHUSU KUBAKI AU KUSEPA LIVEPOOL MSIMU UJAO ...SALAH KAVUNJA UKIMYA...KAFUNGUKA ANACHOHITAJI KWA SASA...