Home YAN YANGA WATAJA SABABU ZA MWANANCHI MEDIA DAY

YANGA WATAJA SABABU ZA MWANANCHI MEDIA DAY


 MSHAURI ndani ya Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko, Senzo Mazingisa leo Feburuari 2, 2021 ametaja sababu tatu za klabu yao kuandaa siku maalum ya vyombo vya habari katika kambi yao ya AVIC Town iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Senzo amesema sababu ya kwanza ni kutoa fursa kwa wanahabari kujua na kuzungumza mambo ya mahusiano kati ya klabu yao na wadhamini wao.

 

“Siku zote Yanga ikicheza nafasi ya kuzungumza huwa kwa makocha, wachezaji wanafanya vizuri na kama ukiwa na bahati utaongea na nahodha.


“Leo ni tofauti nawaona wawakilishi wa wadhamini wetu SportPesa, GSM, Afya, Taifa Gas muwaulize leo kwanini wanaidhamini Yanga na kuendelea kuwapa pesa.

 

“Senzo amesema sababu ya pili ni kutoa nafasi kwa waandishi kujua mazingira ya kambi yao iliyopo Kigamboni na kujua mazingira yake na tatu ni kuzidisha umoja kati ya Yanga na Waandishi wa Habari na kuwa karibu na mashabiki,” .


SOMA NA HII  'SURE BOY' AVUNJA UKIMYA YANGA...'ATAPIKA NYONGO' KISA KUWEKWA BENCHI....ATOA MSIMAMO HUU...