Home Simba SC JONAS MKUDE AREJEA MAZOEZINI BAADA YA KUKOSA MECHI NANE

JONAS MKUDE AREJEA MAZOEZINI BAADA YA KUKOSA MECHI NANE

 HATIMAYE Jonas Mkude amerejea kikosini kuungana na wachezaji wenzake baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake kutokana na utovu wa nidhamu.

Mkude leo Februari 2 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kusimamishwa na Kamati ya nidhamu ya Simba Desemba 28,2020.

Tayari alikuwa amekosekana kwenye jumla ya mechi nane ambazo Simba walicheza ndani ya uwanja, zama zile za Sven Vandenbroeck alikosekana kwenye mechi tatu ndani ya uwanja.

Moja ilikuwa ya Kombe la Shirikisho,  moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika na moja ilikuwa ya Ligi Kuu Bara kabla hajabwaga manyanga Januari 7 na kuibukia Morocco. 

Ikiwa chini ya Kaimu Kocha, Seleman Matola amekosekana kwenye mechi nne ilikuwa ni za Kombe la Mapinduzi,  Visiwani Zanzibar ambapo mabingwa ni Yanga baada ya kushinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Simba kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Amaan.

Mbele ya Didier Gomes mrithi wa Sven amekosekqna kwenye mechi mbili za Simba Super Cup ambapo aliwakosa Al Hilal na TP Mazembe na mabingwa wakawa Simba.

Jumla amekosekana kwenye mechi nane za Simba ndani ya uwanja kiungo huyo mkabaji kipenzi cha mashabiki.

Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa Mkude ni mchezaji wa Simba na makosa ambayo aliyafanya ni ya kibinadamu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA 'KUBUTULIWA' MOROCCO...MBRAZILI SIMBA APEWA 'KONGOLE'....