Home Habari za michezo TETESI:- CHAMA ATAKA MIL 770 KUONGEZA MKATABA MPYA SIMBA….MABOSI WAKUNA KICHWA….

TETESI:- CHAMA ATAKA MIL 770 KUONGEZA MKATABA MPYA SIMBA….MABOSI WAKUNA KICHWA….

Habari za Simba leo

WAKATI Simba wakiendelea kuwaongezea mkataba baadhi ya wachezaji wao, kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameweka mezani ofa yenye thamani ya Dolla za kimarekani laki tatu ili kuongeza mkataba wa kusalia ndani ya klabu hiyo .

Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kuwa kulingana umri wake dau hilo haliwezi kulitoa na kuweka ofa yao mezani na akidhirika nao atakaa mezani kuzungumza na kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya Simba.

Taarifa zilizopatikana jana kuwa mazungumzo baini ya uongozi wa Simba na Chama ilikuwa kuendelea kubaki ndani ya timu hiyo kwa msimu mwingine na kumuongezea mkataba wa miaka miwili.

“Kutokana na Simba kuweka ofa (hakuweka wazi ni kiasi gani), mezani mchezaji huyo ametaka dau kubwa dolla laki tatu (sawa na mill 774) wamegoma kutoa kiasi hicho na akiendelea na msimamo huo wamemuambia hawataweza kuendelea naye,” amesema mtoa habari huyo.

Ameleza kuwa wanahitaji kufanya maboresho makubwa ndani ya timu hiyo, tayari viongozi wanaendelea kuzungumza na baadhi ya wachezaji kutoka klabu tofauti ya nje na ndani ya Tanzania.

“Kwa sasa mazungumzo yanaendelea baini ya uingozi wa Ihefu FC kwa ajili ya kupata huduma ya kiungo Marouf Tchake kwa makubalia ya kutoa (50k USD) na Luis Miquisson kujiunga na timu hiyo.

Lengo la kumtaka Tchake kuja Simba kuchukuwa nafasi ya Saido Ntibazonkiza ambaye hataongezewa mkataba baada ya msimu huu kufikia ukingoni ,” ameema chanzo hicho.

Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema licha ya kutafuta nafasi ya pili na kwenda kucheza ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao lakini wapo katika hatua za kuwaongezea mikataba baadhi ya nyota wao ambao wanatakiwa kusalia ndani ya timu.

Amesema kuna baadhi tayari wameongezewa na wengine wapo kwenye mazungumzo atakayeridhika na ofa yao watahakikisha wanambakiza na asiyeridhika watampa baraka zote anapopata kile anachokihitaji.

“Tuko katika vita vya kusaka nafasi ya pili lakini hii haitatufanya tusianze kuangalia mahitaji yetu kwa wachezaji wapya ambao tutawasajili, fedha ipo tunaenda sokoni kuangalia mahitaji yetu kwa kufuata mapendekezo ya benchi la ufundi ili kuimarisha timu yetu kwa msimu ujao,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA KUANZA 'TIZI' LA KUWASAMBARATISHA MAZIMA WABOTSWANA KESHO