Home Habari za michezo PAMOJA NA SIMBA ‘KUBUTULIWA’ MOROCCO…MBRAZILI SIMBA APEWA ‘KONGOLE’….

PAMOJA NA SIMBA ‘KUBUTULIWA’ MOROCCO…MBRAZILI SIMBA APEWA ‘KONGOLE’….

Habari za Simba leo

KOCHA msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Liogope amemvulia kofia kocha mkuu wa Simba SC baada ya kuangalia namna ambavyo alikuwa bora kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad Casabalanca.

Simba SC ilifungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare 1-1.

Liogope alisema aliuangalia mchezo kwa ukaribu na kugundua kabisa Robertinho ni kocha wa mbinu na ndio maana aliweza kuhimili mchezo kwa dakika 90 kisha akatolewa kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.

“Unajua ukiangalia kwanza hata kufanya mabadiliko walikuwa anachelewa lakini ukijiuliza kama kocha utaona kabisa wale waliokuwepo uwajani walikuwa na nguvu kwa kiasi kikubwa;

“Fitinesi yao ilikuwa kubwa pia na ukiangalia nje kwenye benchi pale ni kweli kuna wachezaji wana uzoefu lakini fitinesi ya mechi kwao ni ndogo na ndio maana alichelewa hata kuingia kwa Erasto (Nyoni).”

Liogope alisema Robertinho kwa sababu alikuwa ugenini alikuwa anafanya mashambulizi ya kushtukiza huku wenyeji wao (Wydad) wao walikuwa wanataka kuimaliza mechi mara moja.

“Wydad ilitaka kumaliza mechi lakini Simba ilituliza mchezo na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, Chama (Clatous) unaweza sema alikuwa haonekani lakini mbinu ilimlazimu ashuke na kukaba na alifanya hivyo.”

SOMA NA HII  IKIWA HAJAMALIZA HATA MIEZI MITATU TOKA ASAJILIWE....NABI AANZA KULIA NA UWEZO WA MORRISON...AMPA 'MAKAVU LIVE'...