Home Uncategorized DAYNA NA PATORANKING WANA JAMBO LAO

DAYNA NA PATORANKING WANA JAMBO LAO


 MWANADADA mwenye kipaji kikubwa kunako gemu ya Bongo Fleva hapa nchini, Dayna Nyange amefunguka kuwa yuko kwenye maandalizi kabambe ya kudondosha ‘sapraizi’ kubwa kwa kushirikiana na staa wa muziki kutokea nchini Nigeria, Patrick Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’.

 

Dayna, mama wa mtoto mmoja amewahi kutamba na ngoma kali kama; Angejua, Komela akiwa na Billnass na Nivute Kwako aliyomshirikisha mkali wa sauti, Barnaba Boy.


Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutokea nchini Nigeria alipokuwa kwenye ziara binafsi, Dayna alisema mashabiki wake wakae mkao wa kula kutokana na ‘project’ kali zinazotarajia kushuka hivi karibuni.

 

“Nimekuwa kwenye ziara yangu binafsi hapa Nigeria ambayo imekuwa na lengo la kujifunza kwa kujionea wenzetu wanafanya nini katika kiwanda cha muziki ambacho kinawafanya wazidi kufanikiwa.

 

“Pamoja na hayo kulikuwa na plani ya kufahamiana na mastaa wa Nigeria ambao tumekuwa tukiwasiliana tu bila kuonana na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hilo kwani nimeweza kukutana na Patoranking, D’banj na meneja wa Wizkid.

 

“Patoranking ni mtu poa na kuna vitu vingi ambavyo tumefanya pamoja vinakuja ila nisingependa kusema mengi kwa sasa bali wakati utakapofika mashabiki wangu watajua ni ‘sapraizi’ gani nawaandalia.”

SOMA NA HII  MASAU BWIRE: ILIBIDI TUWAFUNGE SIMBA MABAO 8-0, BAHATI YAO