Home Uncategorized AZAM FC: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA

AZAM FC: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa una kazi kubwa ya kufanya msimu huu wa 2020/21 kutokana na ushindani uliopo ndani ya Ligi Kuu Bara.


Kwa sasa Azam FC inashika namba moja kwenye msimam baada ya kucheza mechi sita na imeshinda zote.


Safu yake ya ushambuliaji imetuia jumla ya mabao 12 huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili ndani ya dakika 540.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:-“Ushindani ndani ya ligi ni mkubwa na kila timu ipo vizuri hasa inapoingia uwanjani hesabu zake ni kupata pointi tatu kama ambavyo sisi tunahitaji pia tukiwa ndani ya uwanja.


“Kikubwa kwa sasa ni kuona kwamba kila siku tunapata matokeo mazuri na kuendelea kuweka rekodi kwani hakuna timu ambayo haipendi kupata matokeo mazuri.


“Tunapenda kuwashukuru mashabiki wetu pamoja na wachezaji kwa namna wanavyotimiza majukumu yao ndani ya uwanja bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi ambayo tunayafanya,” amesema.


Azam FC kibindoni imekusanya pointi 18 ikifuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 13 sawa na Yanga iliyo nafasi ya tatu tofauti ikiwa ni kwenye mabao ya kufunga na kufungwa, Yanga imefungwa bao moja na kufunga mabao saba huku Simba ikifungwa mabao mawili na kufunga mabao 14.

SOMA NA HII  KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO