Home Uncategorized TUSIACHE KUPUUZIA ISHU YA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI HUU WA MAPAMBANO DHIDI YA...

TUSIACHE KUPUUZIA ISHU YA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI HUU WA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA


SIE wabongo tumekuwa wagumu sana kukubaliana na jambo flani linapotokea hasa lile la mabadiliko.
Yaani swala la mabadiliko ni gumu kulikubali na hapa utasikia wabongo hilo litakwama tu.

Na kweli kwenye soka letu kuna mengi mazuri yamekwama kwasababu tu ya wachache wanajiona watu wa soka hawayapendi.
Sasa Serikali inawaonyesha kuwa yenyewe ni kubwa na ina mkono mrefu kuliko chochote kwenye hii nchi.
Jamani, Corona haijamalizika ila imepungua kwa kiasi kikubwa hivyo tupunguze misongamano lakini sie tunaojiita mashabiki kweli kweli hatutaki kusikia wala kuambiwa.
Tayari timu pendwa za Simba na Yanga zitacheza bila ya mashabiki kwenye michezo yao yote iliyosalia kwenye viwanja vya mikoani.
Hapa hakuna wa kumlaumu wenyewe ndio mnastahili lawama kwasababu hamkutaka kusikia.
Huko Ulaya kwenye teknolojia mashabiki wamezuiwa kuingia viwanjani lakini hapa kwetu ni kama msaada tu umetolewa kwa mashabiki lakini wamekuwa wagumu kuelewa.
Kingine viongozi wengi wa soka hapa kwetu wanajua zikicheza Simba na Yanga ni muda wa mavuno hawajali chochote kwao mavuno mbele hakuna kingine.
Sasa niwape pole maana mavuno hayapo tena maana Serikali imerefusha mkono wake na kupiga kufuri hakuna mashabiki na sijui sasa watavuna kitu gani.
Kiufupi tunatakiwa kuongeza umakini kwenye uongozi wa soka kuanzia chini kabisa hadi juu sio kuwalaumu TFF tu hapana wako wengi wa kulaumiwa na kama hili TFF hawahusiki kabisa hapa ni vyama vya mikoa na vilabu.
Tujifunze kuelewa mambo jamani tusipende kuenda kama tulivyozoea maana dunia imebadilika na sisi twende kama ilivyo.
Kila mmoja na awe mlinzi wa mwenzake kwa kuwa fedha zipo siku zote na huwa haziishi ila afya ni jambo la msingi ambalo linapaswa lichukuliwe umakini mkubwa.
Ile fungiwa ya JKT Tanzania baada ya kukiuka muongozo kwa kuruhusu mashabiki wengi ndani ya uwanja ilipaswa kuwa somo kwa wengine.
Ajabu ni kwamba kutokana na ubishi wa wengi hasa mashabiki kutaka kuyapeleka mambo kwa mazoea kunafanya mambo mengine yatokee kwa wengine pia.
Hii fursa ilikuwa ni lazima kwenda nayo kwa akili kubwa huku tukiamini kwamba ili kuilinda ilikuwa ni lazima kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali.
Ni jambo la msingi kutii wenye mamlaka kwa kufuata utaratibu ambao umewekwa kwani hakuna haja ya kupuuzia ilihali kila kitu kipo wazi kwa haya yanayotokea ni lazima tujifunze wakati mwingine ikitokea taarifa ni muhimu kuifanyia kazi.
Tuna kazi ya kupambana na adui Corona huku tukiamini kwamba maambukizi yamepungua ila haina maana kwamba taratibu zote zirudi kama awali hapana ni muhimu kuwe na mabadiliko.
Kwa kufanya hivyo itatusaidia kuweza kulinda afya za kwetu wenyewe kabla ya kupigiwa kelele na Serikali ambayo inaamini kwamba muongozo uliotolewa una maana kubwa.

SOMA NA HII  HASSAN MWAKINYO ABEBA UBINGWA WA DUNIA