Home Habari za michezo KOCHA WA SIMBA SC KUKUTANA NA YANGA NUSU FAINAL CAF…WASAUZI MENO NNJEE…

KOCHA WA SIMBA SC KUKUTANA NA YANGA NUSU FAINAL CAF…WASAUZI MENO NNJEE…

Habari za Simba SC

Unaemuona hapo anaitwa Dylan Kerr! Ndiye Kocha Mkuu wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, timu itakayocheza na Yanga SC kwenye hatua ya Nusu Fainali ya CAFCC.

Dylan Kerry amewahi kuifundisha Simba SC msimu wa 2015/2016 kisha akaenda Gor Mahia alikokaa mwaka mmoja halafu tangu hapo kaenda Afrika Kusini ambako yupo mpaka sasa na amepita timu 4 hii ya 5 (Black Leopards, Baroka, Tshakhuma, Moloka Swallows na sasa Gallants).

Mwaka 2021 wakati Kaizer Chiefs wanakuja kucheza na Simba SC mchezo wa marudiano wa CAFCL Dylan Kerry kipindi hicho akiwa Kocha wa Tshakhuma Tsha Madzivhandila alinukuliwa akiwatahadharisha Kaizer Chiefs kwamba ameishi Tanzania, anazijua Timu za Tanzania hivyo Kaizer Chiefs wasiingie Dressing Room kwakuwa Timu za Tanzania hasa Simba wako tayari kufanya chochote ili wapate ushindi.

Muhimu, Yanga wa-focus kwenye maandalizi ya michezo yote miwili, wanao uwezo wa kufanya hivyo bila hata kushauriwa na ninawatakia heri Wananchi waweze kufika fainali na hata kutwaa Ubingwa wa CAFCC.

Cha ajabu sasa, Marumo Gallants wako nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini lakini Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Tanzania Bara mpaka sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 68 na kuna uwezekano mkubwa wa kubeba taji hilo tena.

SOMA NA HII  KUHUSU KUIFUNGA JWANENG ...SHABIKI SIMBA AMLIPUA AHMED ALLY..."ANATUDANGANYA HUYU"...