Home Habari za michezo KWA TWAKWIMU HIZI ZA YANGA MSIMU HUU CAF….WASIPOCHUKUA UBINGWA WAMELOGWA…

KWA TWAKWIMU HIZI ZA YANGA MSIMU HUU CAF….WASIPOCHUKUA UBINGWA WAMELOGWA…

Habari za Yanga SC

Klabu ya Yanga SC si kwamba imefuzu tu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, bali imeongoza katika vitu vingi kwenye michuano ya CAFCC mwaka huu.

Yanga SC ambayo  imetinga nusu fainali baada ya kuiondoa Rivers United, imeandika rekodi ya aina yake katika michuano hiyo mpaka sasa.

Yanga SC imekuwa timu ya kwanza Tanzania kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu lianzishwe mwaka 2004.

Timu zenye clean sheets nyingi mpaka sasa. 05 – Young Africans 05 – ASEC Mimosas 04 – US Monastir

Michezo (5) ya mwisho (CAF) Yanga 2 – 0 Bamako Yanga 2 – 0 US Monastir Yanga 1 – 0 TP Mazembe – (A) Yanga 2 – 0 Rivers – (A) Yanga 0 – 0 Rivers

Timu zilizofanya vizuri zaidi kwenye mechi (5) za mwisho CAFCC.

1. Ushindi 4, sare 1, kupoteza 0, tofauti ya mabao +7, alama 13 – Yanga Sc 2. Ushindi 4, sare 1, kupoteza 0, tofauti ya mabao +6, alama 13 – ASEC Mimosas 3. Ushindi 3, sare 1, kupoteza 1, tofauti ya mabao +9, alama 10 – USM Alger

Magolikipa wenye cleansheets nyingi! 05 – Ayayi Charles 04 – Djigui Diarra

Vinara wa magoli! ⚽ 05 – Fiston Mayele ⚽ 05 – Chivaviro

SOMA NA HII  BAADA YA KUINA YANGA IKITESEKA JUZI DHIDI YA NAMUNGO...KAZE ATIKISA KICHWA KISHA AFUNGUKA HAYA..