Home Habari za michezo KISHA USHINDI WA YANGA SC CAF….MZEE YUSUF ASHINDWA KUJIZUIA….AFUNGUKA HAYA KWA WANIGERIA….

KISHA USHINDI WA YANGA SC CAF….MZEE YUSUF ASHINDWA KUJIZUIA….AFUNGUKA HAYA KWA WANIGERIA….

Habari za Yanga SC

Msanii maarufu na nguli wa muziki wa Taarabu, Mzee Yusuf ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga SC, amesema kuwa kwa sasa klabu hiyo haina presha na michuano mikubwa ya CAF kwani imeonyesha inao uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa zaidi barani Afrika.

Mzee Yusuf amesema hayo wakati akihojiwa na vyombo vya habari mara baada ya yanga SC kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga Rivers United.

“Yanga SC tumeweka historia, historia huandaliwa, huandikwa na kuwekwa, historia ndiyyo inawafanya watoto miaka ijayo watoto watasoma na kujua Yanga ilikuwa hivi. Ni historia ya kibabe sana kumpiga kwao, akaja hapa tukamwachia afunge akashindwa.

“Haya ni mashindano makubwa wala sio ya Lipa Nikulipe, kocha Nabi aliweka plan yake kuhakikisha hawashindi sababu tulikuwa na ushindi wa bao 2-0 mkononi. Ndiyo maana wachezaji wetu wengi walikuwa wametulia tu.

“Hakuna shabiki wa Yanga aliyekuwa na presha kwamba labda tutafungwa hayupo. Yanga imeweka plan yake kufanya mambo makubwa katika mashindano makubwa. Sisi hatuna malengo ya fainali, malengo yetu tumalize kwanza nusu fainali ndipo tutaweka malengo ya fainali,” amesema Mzee Yusuf.

Yanga itakutana na Marumo Gallants katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza utapigwa katika dimba la Mkapa, Mei 10, 2023 kisha mchezo wa marudiano utapigwa nchini Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu.

SOMA NA HII  KISA 'KUILOGA' SIMBA...TFF WAISHUSHIA RUNGU LA ADHABU SINGIDA BIG STARS...