Home Habari za michezo BAADA YA KIMYA KIREFU….AJIBU KASHINDWA KUJIZUIA…KAIBUKA NA HILI JIPYA KWA TIMU YAKE…

BAADA YA KIMYA KIREFU….AJIBU KASHINDWA KUJIZUIA…KAIBUKA NA HILI JIPYA KWA TIMU YAKE…

Ajibu akiwa Singida Big Stars

Kiungo Mshambuliaji wa Singida Fountain Gate FC, Ibrahim Ajibu, ameendelea kuimarika kutokana na majeraha aliyokuwa nayo hali iliyompelekea kukaa nje kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ajibu amesema kwa sasa anaendelea vyema na tayari ameanza kufanya mazoezi mepesi.

“Ninashukuru hali yangu inaendelea vizuri baada ya kukaa nje muda mrefu ninaamini msimu ujao nitakuwa nimeimarika zaidi, amesema Ajibu

Amesema maendeleo yake ya sasa yanampa matumaini ya kuanza mazoezi mapema ya kujiweka sawa kuelekea kwenye msimu ujao ambao ameahidi kufanya vizuri zaidi.

Mshambuliaji huyo amesema alishindwa kuonyesha makali yake msimu uliopita kufuatia majeraha hayo na kuahidi kuendeleza kiwango chake.

“Nitarudi tu kwenye kiwango changu, kikubwa ilikuwa kupona kwanza, nashukuru Mungu hali yangu ya sasa, nimeanza mazoezi mepesi na ndani ya muda mfupi nitarejea kwenye mazoezi ya nguvu kabla ya kuanza maandalizi na timu yangu kuelekea kwenye msimu mpya,” amesema Ajibu

Ajibu alijiunga na Singida Big Stars (Sasa Singida Fountain Gate) msimu uliopita akitokea Azam FC ambapo hakupata nafasi kubwa ya kucheza.

SOMA NA HII  WIKI YA WANANCHI YANGA..TAREHE YATANGAZWA...KUPISHANA ANA SIMBA DAY KWA SIKU MBILI TU...