Home Uncategorized SIMBA WAJANJA KWELI WAMUWAHI YULE MTUPIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA

SIMBA WAJANJA KWELI WAMUWAHI YULE MTUPIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA


INAELEZWA kuwa Uongozi wa Simba umeamua kumalizana na mchezaji wao Deo Kanda ambaye alikuwa kwenye hesabu za kutua ndani ya Yanga msimu ujao.

Kanda ambaye alitua Bongo akitokea Congo kwa mkopo wa muda wa mwaka mmoja ambapo msimu ukimeguka naye dili lake lilikuwa linameguka ameongezewa dili jingine.

Habari zinaeleza kuwa kutokana na mchango wake kuwa mkubwa ameongezewa kandarasi ya miaka miwili ili abaki ndani ya Simba.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alipotafutwa azungumzie suala hili hakuwa tayari kuweka wazi.

Kanda amefunga mabao saba ndani ya Simba ambayo imefunga jumla ya mabao 63 kwenye Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  SIMBA YAAGIZA STRAIKA WA KIMATAIFA