Home Uncategorized SIMBA:LIGI KUU INA USHINDANI MKUBWA

SIMBA:LIGI KUU INA USHINDANI MKUBWA


BEKI Kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ina ushindani mkubwa jambo ambalo linawafanya wapasue kichwa kusaka matokeo ndani ya uwanja.
Simba ikiwa imecheza mechi 28 imefungwa mabao 15 ambayo ni machache kwa msimu huu kwa timu ambazo zimecheza mechi 28 ndani ya ligi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa wamekuwa na kazi ngumu ya kufanya kwa pamoja kulinda lango na kutafuta ushindi kutokana na timu nyingi kuwa kwenye ubora.
“Ushindani wa ligi ni mkubwa na kila timu inatafuta ushindi hilo linafanya nasi tuwe kwenye wakati mgumu pale tunaposhindwa kupata ushindi, kwa sasa tunaendelea kutazama mechi zetu zinazokuja zile zilizopita hatuwezi kubadili matokeo yake,” amesema.
Mchezo wao wa Machi 8 mbele ya Yanga walikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ikiwa ni baada ya miaka mnne kupita bila kufungwa na watani zao hao wa jadi.
SOMA NA HII  HIZI NDIZO SEHEMU AMBAZO TIKETI ZA MECHI SIMBA NA UD SONGO ZINAUZWA