Home Uncategorized CORONA YASIMAMISHA LIGI KUU ENGLAND KWA MUDA

CORONA YASIMAMISHA LIGI KUU ENGLAND KWA MUDA



LIGI Kuu ya England imesimamishwa kuanzia leo Machi 13 kwa muda wiki mbili inatarajiwa kurejea Aprili 3 kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

Hatua hii imefikia baada ya Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta kungundulika na Virusi hivyo baada ya kufanya vipimo.

Ligi Kuu ya England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Legue One, League Two, FA ya Wanawake na Wanaume, Europa League hizi zote zimesimamishwa kuanzia leo kutokana na Virusi vya Corona.

Miongoni mwa waliogundulika na Corona ni pamoja na nyota wa timu ya Chelsea, Callum Hudson-Odoi ambaye amesema kuwa kwa sasa anaendelea vema kufuata kanuni za afya.

SOMA NA HII  YANGA YAWAOMBA MASHABIKI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI