Home Habari za michezo DUNIA YA TIKISIKA NA USAJILI WA ANTONY KWENDA MAN UTD…ZAIDI YA BIL...

DUNIA YA TIKISIKA NA USAJILI WA ANTONY KWENDA MAN UTD…ZAIDI YA BIL 233 ZAYEYUKA KIULAINII KABISA…


Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa winga Antony Raia wa Brazil kutoka klabu ya Ajax ya Uholanzi na atasaini mkataba wa miaka 5 wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Antony anajiunga na Manchester united kwa ada ya uhamisho ya pesa za Uingereza pauni million 85.5 ambayo ni zaidi ya bilioni 233 na milioni 393 kwa pesa ya Tanzania. The Red Devils watalipa pesa hiyo kwa awamu mbili awamu ya kwanza watalipa Pauni million 81.3 na awamu ya pili watalipa pauni milioni 4.2.

Huu ni usajili wa tano (5) Manchester United wanakamilisha kwenye dirisha hili kubwa la usajili la majira ya joto barani Ulaya ambalo rasmi litafungwa Septemba 1, 2022. Wachezaji wengine waliosajiliwa ni Tyrell Malacia, Christian Eriksen, Lisandro Martinez na Casemiro.

Winga huyo raia wa Brazil ana umri wa miaka 22 akiwa na klabu ya Ajax amefunga mabao 24, ametoa pasi za kufunga mabao (Assists) 22 kwenye michezo 82. Lakini pia akiwa na kikosi hicho ameshinda mataji 3 ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu Uholanzi Eredivisie mara mbili.

SOMA NA HII  SIMBA WAMBEBA MSHAMBULIAJI HUYU WA AZAM FC