Home news TWIGA HESABU ZAO NI KUTWAA TAJI LA COSAFA

TWIGA HESABU ZAO NI KUTWAA TAJI LA COSAFA


WACHEZAJI na benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars wamesema kuwa kuna asilimia 80 ya kuwashinda Malawi na kutwaa kombe la Cosafa.

Twiga Stars leo majira ya saa 10:00 alasiri, watacheza mchezo wa Fainali dhidi ya Malawi Uwanja wa Nelson Mandela.

Twiga walitinga fainali hiyo baada ya kuwachapa Zambia kwa penati 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Kocha wa timu hiyo Bakari Shime aliliambia amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari na wanahitaji kupata ushindi.

“Kazi kubwa msimu huu itaonekana ya thamani zaidi kama tutapata matokeo kwenye mchezo huu wa fainali imani yangu inasema tutashinda.

“Wachezaji wapo tayari na tunaamini kwamba hata Watanzania wanajua kwamba tunahitaji ushindi, kila kitu kitakuwa sawa,” .


SOMA NA HII  BAADA YA KUMSHUSHA OKRAH....YANGA WARUDI TENA GHANA SAFARI HII KIFAA HIKI KINASHUKA...