Home Habari za michezo GAMONDI ATUMIA DIRISHA DOGO KUWANYOOSHA MASTAA YANGA

GAMONDI ATUMIA DIRISHA DOGO KUWANYOOSHA MASTAA YANGA

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Gamondi amewatega wachezaji wake kwa kuwaambia kuwa mchezaji atakayeshindwa kuonyesha kiwango bora katika Kombe la Mapinduzi, basi safari itamkuta katika usajili huu wa dirisha dogo.

Kocha huyo kutoka Argentina amepanga kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kucheza katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji baadhi wanaoatajwa kuachwa na timu hiyo, ni Jonasi Mkude, Jesus Moloko, Chrispin Ngushi, Gift Fred na Denis Nkane ambaye anatajwa kupelekwa kwa mkopo Dodoma Jiji.

Gamondi amesema kuwa muda muafaka wa wachezaji ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika ligi na michuano ya kimataifa, muda wao sasa kumuonyeshea ubora wao katika Kombe la Mapinduzi.

Gamondi amesema kuwa, amepanga kusafiri na wachezaji wote tofauti na wale ambao watakaokuwepo katika majukumu ya timu zao za taifa, kwa lengo la kutoa nafasi ya kuwaangalia kabla ya kuchukua maamuzi ya kuachana na baadhi ya wachezaji.

Ameongeza kuwa wachezaji hao wanatakiwa kumshawishi kwa kuonyesha viwango bora, ambavyo vitamshawishi kumbakiza katika dirisha hili dogo.

“Sitakuwa na udhuru na mchezaji yeyote, badala yake nitasafiri na wachezaji wote kwenda Zanzibar kucheza Kombe la Mapinduzi katika msimu huu.

“Nimepanga kutoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji ambao walikosa nafasi ya kucheza katika ligi na michuano ya kimataifa, lengo kuona ubora wa kila mchezaji kabla ya maamuzi sijayachukua katika dirisha hili dogo.

“Ni muda wa wachezaji hao kunishawishi kwa kuonyesha kiwango bora, ambacho kitakachowabakisha Young Africans katika msimu huu,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA ISHU YA KONKONI KUANZIA BENCHI