Home Habari za michezo MWAMBA HUYU HAPA ASAINI MIAKA MIWILI

MWAMBA HUYU HAPA ASAINI MIAKA MIWILI

Habari za Simba

Winga wa zamani wa Simba, Augustine Okrah sasa ni rasmi ametua Yanga, huku taarifa za ndani zikidaikuwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Juzi ziliibuka taarifa za nyota huyo raia wa Mghana kuhusishwa na Yanga na jana vyanzo vya uhakika kutoka karibu na mchezaji huyo pamoja na Yanga vikisema jamaa huyo ameshamalizana namabosi wa Jangwani kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ili kuitumikia timu hiyo na mashabiki watamuona kwenye michuano ya Mapinduzi 2024.

Kiungo huyo mshambuliaji aliyechezea Simba msimu wa 2022/23 na kushindwa kudumu baada ya kuondoka kwenye dirisha kubwa lililopita akiwa na mabao manne na asisti moja, anakumbukwa zaidi kwa bao safi aliloifunga Yanga kwenye mchezo wa Kariakoo Derby ulioisha kwa sare ya bao 1-1, Oktoba 23, 2022 kisha akavua jezi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimelithibitishia Mwananchi kuwa winga huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na ataonekana uwanjani kwenye mchezo wa kundi C dhidi ya Jamhuri Desemba 31.

“Ni kweli kama watu wanavyosema Okrah yupo na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga. Uongozi nafikiri utamtambulisha Desemba 30 usiku au kabla ya hapo kwa kuwa atakuwa na timu kwenye Mapinduzi,” kilisema chanzo hicho.

“Kocha Miguel Gamondi aliomba kupewa winga mmoja mwenye kasi na nguvu na alipoelezwa kuhusu Okrah akaridhia ndiyo maana akapewa mkataba.”

Tangu alipotua Bechem United ya Ghana akitokea Simba, nyota huyo amefunga mabao tisa katika mechi 15, akilingana na Isaac Mintah wa Aduana.

“Okrah ni mchezaji mzuri na Yanga ilivyo sasa ina wachezaji wengi wenye ubora. Kama watampa nafasi atafanya kitu kikubwa kama alivyofanya kwenye timu ambayo alikuwa anaitumikia sasa akiwa ni kinara wa ufungaji,” alisema rafiki wa karibu wanyota huyo.

Hata hivyo, Mwananchi lilimtafuta ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe kuzungumzia taarifa hiyo, lakini hakupatikana kwani simu zake hazikupokewa.

ATACHEZA WAPI?

Wakati Okrah akitajwa kumalizana na Yanga nyota huyo atahatarisha vibarua vya baadhi ya wachezaji kutokana na kumudu kucheza nafasi hizo, huku pia akiwa ni mchezaji ambaye atasaidiana na utatu wa Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzou na Maxi Nzengeli kutokana na nafasi hizo pia kuwa na uwezo nazo.

Okrah anaweza kucheza nafasi tatu uwanjani kama winga wa kulia na kushoto na pia anaweza kucheza kama mahambuliaji namba 10 – eneo ambalo limekuwa na wachezaji wanaofanya vizuri kwa sasa wakiongozwa na Aziz Ki aliyetupia mabao 10 kwenye ligi.

Katika winga za pembeni Jangwani ni dhahiri anakwenda kumpa changamoto Jesus Moloko ambaye amekuwa akitumiwa zaidi eneo hilo sambamba na Kennedy Musonda, hivyo nyota hao watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanapambania namba zao.

Kutokana na hali hiyo huenda Yanga wakalazimika kumuacha mchezaji mmoja ili Okrah aingie kwenye usajili, huku Hafiz Konkoni na Gift Fredy wakionekana kukalia kuti kavu.

SOMA NA HII  AZAM FC WAIBUKIA HUKU KWA SASA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI WAO