Home Uncategorized AZAM FC WAIBUKIA HUKU KWA SASA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI WAO

AZAM FC WAIBUKIA HUKU KWA SASA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI WAO



UONGOZI wa Azam FC umewaomba mashabiki waendelee kuipa sapoti kila wakati bila kukoma licha ya kupitia kipindi cha mpito.


Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na pointi 45 imecheza mechi 24 huku kinara akiwa ni Simba wenye pointi 62.

Kwenye mechi zake tatu za mwisho ilipokuwa ikisaka pointi tisa imeambulia pointi moja na kupeperusha pointi nane.

Ilianza kuchapwa mabao 2-1 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Uhuru, ikalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda kabla ya kukubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Namungo FC.

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa:”Mashabiki tunawaomba waendelee kutupa sapoti kwani uwepo wao unatufanya tuendelee kupata nguvu ya kupambana,”.
SOMA NA HII  DILI LA MWAMNYETO YANGA LIMEFIKIA HAPA