Home Uncategorized KAGERE ATAJA SABABU YA KUFUNGA MABAO NDANI YA LIGI KUU BARA

KAGERE ATAJA SABABU YA KUFUNGA MABAO NDANI YA LIGI KUU BARA

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anafunga kwa kuwa ni kazi yake na malengo yake kuendelea kufunga kila anapopata nafasi.

Simba ikiwa imefunga mabao 50, Kagere amehusika kwenye mabao 19. Amefunga 14 na kutoa pasi za mwisho tano.

Kesho atakuwa na kazi ya kukiongoza kikosi kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United, Uwanja wa CCM Kambarage.

Kagere amesema:-“Ninamshukuru Mungu kwa kuwa ninapata nafasi ya kufunga na malengo yangu ni kuona ninaendelea kufunga kila ninapopata nafasi, nafanya kwa sababu ni kazi yangu,”.

SOMA NA HII  LIPANGILE WA KMC AWAPIGA BAO WADADA WA AZAM NA DILUNGA WA SIMBA