Home Habari za michezo BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAMTAKA…’STRAIKA’ LA KAZI LAKATAA KUSAINI MKATABA MPYA…

BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAMTAKA…’STRAIKA’ LA KAZI LAKATAA KUSAINI MKATABA MPYA…


Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa, Mshambuliaji wa Vipers ya Uganda, Cesar Manzoki, amegoma kusaini mkataba aliopatiwa na timu yake, huku Simba wakihusishwa katika mpango huo.

Manzoki ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba, hivi karibuni aliweka wazi yupo katika mazungumzo na timu hiyo na tayari amepewa mkataba wa awali ambao bado hajausaini.

Mshambuliaji huyo amesema baada ya Vipers kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitatu, bado hajasaini huku akisema ana asilimia ndogo kusalia ndani ya timu hiyo.

“Kuna asilimia ndogo za mimi kusalia hapa na kuna asilimia kubwa za kuondoka, kuna ofa ninazo ikiwemo ile ya kusalia niliyopewa na uongozi wa timu, pia ofa nyingine ikiwemo ya Simba.

“Hivyo ndani ya siku chache zijazo nadhani nitakuwa nimekamilisha mchakato mwingine ambao utaenda kubadilisha historia yangu katika mpira.

“Ni jambo la subira kwa kuwa ni mambo ya usajili, hivyo huhitaji mpaka mchakato ukamilike ndiyo kujadiliwa, lakini itakuwa mbaya kama tutazungumza jambo halafu dili likashindwa kutimia,” alisema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  MCHAMBUZI RWANDA AZIPA UKWELI SIMBA NA YANGA...."KWA MWENDO HUU HAWAENDI POPOTE"....