Home Habari za michezo KUHUSU MUSTAKABALI WA BEKI MPYA YANGA SC….,UKWELI MCHUNGU NI HUU…,HAKUNA KUPEPESA MACHO…

KUHUSU MUSTAKABALI WA BEKI MPYA YANGA SC….,UKWELI MCHUNGU NI HUU…,HAKUNA KUPEPESA MACHO…

Beki mpya wa Yanga SC Mamadou Doumbia

TUNAJUANA bwana, Yanga SC na Simba haziwezi kumsubiria mchezaji kwa mwaka mzima.

Nawasikia tu baadhi ya watu ndani ya Yanga SC wanavyomtetea Mamadou Doumbia eti ni beki mzuri lakini hajapata nafasi ya kutosha ya kucheza.

Hii nafasi kwani inatolewa kwa upendeleo jamani? Hakuna kocha anayeweza kumuweka nje mchezaji mzuri na kama Doumbia angekuwa na kiwango cha kumridhisha Nasreddine Nabi angepewa tu hiyo nafasi ya kutosha ya kucheza.

Emu tujiulizeni hapa kila mmoja je angekuwa ndio yeye kocha wa Yanga SC angeweza kuwaweka nje Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca ili acheze Doumbia?

Haya tuachane na huyo, huko Simba nako kuna mtu anaitwa Ismail Sawadogo naye anawaangusha kweli viongozi waliomsajili maana kila anapobebwa habebeki.

Mwanzoni alitetewa kwamba sijui hayuko fiti tu kwa sababu hajapata mechi za kucheza kwa muda kidogo lakini sasa uvumilivu unaonekana kuanza kuwashinda hata hao waliokuwa wakimpigania.

Kocha Robertinho kampa sana imani yule mchezaji akiamini kwa kucheza cheza angalau anaweza kurudisha kasi na ufiti lakini wapi bwana weee.

Yeye mwenyewe sasa ameshaanza kumchoka na kama mnavyoona kuna mechi kamuingiza na kumtoa katika kipindi hichohicho cha kwanza maana aliona kabisa kuwa atamharibia kazi yake.

Tunaenda kwenye dirisha kubwa la usajili unafikiri Simba na Yanga ninazozijua mimi zitabaki na hao wachezaji?
Kama wakinusurika nitaamini uchawi upo

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUONGOZA LIGI...GSM AGUNA KISHA AFANYA KUFRU BAB KUBWA HUKO...MWAKALEBELA ATIA NDIMU...