Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…HITIMANA NA KMC YAKE WAOMBA MUNGU AWAKUMBUKE HATA...

KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…HITIMANA NA KMC YAKE WAOMBA MUNGU AWAKUMBUKE HATA NA SARE TU…


Kocha Mkuu wa KMC, Thiery Hitimana amesema mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC wanahitaji pointi ya aina yoyote ili wazidi kukaa sehemu nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Azam na KMC watacheza mechi yao Mei 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:00 usiku.

“Mchezo utakuwa mgumu sana kwa sababu wenzetu wanataka kumaliza zile nafasi tatu hadi nne za juu, sisi pia tunahitaji pointi ili tutoke sehemu tuliyopo maana wale wa chini nao wanataka kusogea juu,” alisema Hitimana.

“Kikosi kipo vizuri na tunaendelea na mazoezi, hatujapata mechi ya kirafiki kwa sababu kuna sikukuu kama hivi lakini hilo halitusumbui sana maana bado tunaendelea na mazoezi yetu kama timu,” alisema Hitimana ambaye ni kocha wa zamani wa Simba na Namungo zilizocheza jana jioni mjini Lindi.

Wakati KMC wakiwa hajapata mchezo wowote ule hivi karibuni, Azam wao wamecheza mechi yao ya ligi jana dhidi ya Kagera Sugar.

Azam wanashika nafasi ya nne (kabla ya mchezo wa jana) wakiwa na pointi 29 katika Ligi Kuu Bara, huku KMC wakishika nafasi ya tisa na pointi 24.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI WOTE KUHUSU ULE UJENZI WA UWANJA MPYA DODOMA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here