Home Habari za michezo KISA UWEZO WA OUATTARA KWENYE MECHI YA JUZI….PAWASA AIBUKA NA HILI JIPYA…AMKUMBUKA...

KISA UWEZO WA OUATTARA KWENYE MECHI YA JUZI….PAWASA AIBUKA NA HILI JIPYA…AMKUMBUKA ONYANGO….


Hivi sasa ndani ya Simba kuna presha kubwa kutoka kwa beki Mkenya, Joash Onyango anayetaka avunjiwe mkataba ili aondoke ndani ya klabu hiyo kutokana vita kubwa ya namba kutoka kwa mabeki wenzake, Henock Inonga na Mohammed Ouattara aliyetua kikosini msimu huu.

Kocha wa Simba, Zoran Maki amekuwa akiwaanzisha Inonga na Quattara tangu mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, hivyo Oyango anaona itakuwa ngumu kwake kupata nafasi ya kucheza licha ya kupewa uhakika wa kucheza mara kwa mara kwenye mkataba wake

Hata hivyo, licha ya baadhi ya mashabiki kuona kama safu ya ulinzi ya Simba haijatulia sana huku wengine wakienda mbali kwa kumtaka kocha kurudisha ile kombinesheni ya Inonga na Onyango lakini beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amemwagia sifa Ouattara kuwa ni mtu na nusu, hivyo watu waendelee kumfuatilia na watakubali kazi yake.

Pawasa ametoa tofauti ya mabeki hao watatu huku akimpa nafasi kubwa Ouattara kucheza pamoja na mmoja kati ya Inonga na Onyango.

“Ujue watu wanashindwa kuelewa kuwa Inonga na Onyango wana aina moja ya uchezaji na wote ni wazuri kwa kufanya makini na mikiki mikiki uwanjani

“Ouattara yeye ni mtu wa mwisho ambaye ni mzuri kwa kuanzisha mashambulizi na kuituliza timu yaani beki huyu anacheza kama namba tano halisi, halafu pia ni mtulivu sana uwanjani, ”alisema Pawasa, beki aliyewahi kuitumia pia Stars.

“Sasa hapo hakuna jinsi kati ya Inonga na Onyango kwa sasa lazima mmoja aanzie bechi tu na mwingine acheze na Ouattara kwani huwezi kuwapanga Onyango na Inonga kwa pamoja ni sana na kumpanga mtu mmoja katika nafasi mbili tofauti kama ilivyokuwa msimu uliopita.

SOMA NA HII  KMC: HATUNA TIKETI YA UBINGWA WA SIMBA