Home Habari za michezo BAADA YA AKPAN NA KAPAMA KUCHEZA JUZI NA KUONYESHA UWEZO WAO….KOCHA SIMBA...

BAADA YA AKPAN NA KAPAMA KUCHEZA JUZI NA KUONYESHA UWEZO WAO….KOCHA SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA HAYA…


Wachezaji wapya wa Simba, Victor Akpan na Nassoro Kapama wamefanikiwa kumshawishi kocha Zoran Minojlovic, ambaye alishindwa kuwapa nafasi katika mechi yoyote ya ligi.

Simba ilicheza na Asante Kotoko ya Ghana nchini Sudan, juzi, ikiibuka na ushindi wa mabao 4-3, huku wachezaji hao wakiwa katika kiwango kizuri cha kumshawishi kocha wao.

Akizungumza jana, kocha Zoran alisema anahitaji kuwapa mechi nyingi Akpan na Kapama kutokana na viwango vyao walivyoonyesha katika mechi hiyo kuwa na mabadiliko makubwa tofauti na awali.

Zoran alisema Akpan alikuwa imara katika eneo la kiungo, alifanya kazi nzuri ya kukaba na kuzuia mashambulizi pamoja na viungo wa timu pinzani na muda mwingine alikuwa akianzisha mashambulizi.

“Kuhusu Kapama, amecheza vizuri katika eneo la beki wa kati pamoja na Henock Inonga kana kwambwa walishawahi kucheza pamoja, ingawa kuna makosa ya kiulinzi aliyafanya ikiwemo ile penalti, lakini mengi yanarekebishika tena kwa haraka,” alisema Zoran.

Katika hatua nyingine, kocha huyo raia wa Serbia alisema kuna makosa yalifanyika kama timu, lakini Akpan na Kapama akiwapa mechi zaidi anaamini watakuwa katika kiwango bora zaidi ya walichoonyesha katika mchezo huo.

Zoran alisema amevutiwa na kiwango alichoonyesha kipa, Ally Salim, kwani hakutegemea kama anaweza kuwa na ukomavu wa aina hiyo katika kuokoa mashambulizi ya wapinzani, alijiamini, aliwapanga mabeki pamoja na utulivu mkubwa kwake.

“Niliamua kutumia mfumo wa 3-5-2 kwani kuna baadhi ya mechi hasa za kimataifa tutahitaji kucheza kwa nidhamu kubwa ya ulinzi kutokana na wapinzani walivyo, zaidi tukiwa ugenini.

“Ushindi katika mchezo huu ni muhimu kwetu kwani utaleta hali ya kujiamini kwa wachezaji na kuendelea kufanya maandalizi kwa hali ya juu kama tulivyokuwa tunahitaji kabla ya kucheza mechi za kimashindano,” alisema Zoran.

Simba inatarajia kushuka tena uwanjani leo ikiwa ni mechi nyingine ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao, Al Hilal ya nchini humo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOTEZA KATIKA MCHEZO ULIOPITA GAMONDI HATAKI UTANI TENA