Home Uncategorized YANGA YAGOMA KUSHUKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA LIGI KUU BARA

YANGA YAGOMA KUSHUKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA LIGI KUU BARA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa malengo yao ni kubaki nafasi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara mpaka mzunguko wa pili utakapomeguka ili watimize malengo yao ya kutwaa ubingwa.


Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 imekusanya jumla ya pointi 31 na haijapoteza mchezo ndani ya ligi zaidi ya kuambulia sare nne.


Ushindi wake mfululizo kwa mechi mbili na mabao yao mawili umeifanya izidi kujijengea ufalme kileleni huku Deus Kaseke akiibuka shujaa kwenye mechi zote mbili mfulukizo ilikuwa mbele ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex na mbele ya JKT Tanzania Uwanja wa Mkapa.


Mechi zote mbili Kaseka alitupia bao mojamoja na kuipa timu yake pointi tatu mazima ambazo zimewafanya wajikite kileleni.


Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:”Sisi ni Wananchi, hatuna presha na kile ambacho tunakifanya zaidi ya kuongeza juhudi ili kupata matokeo chanya.


“Kwa namna ambavyo tunafanya malengo yetu ni kuona kwamba tunabaki kileleni mpaka mzunguko wa pili utakapokamilia ili tutatwae ubingwa,” .


Ubingwa wa Ligi Kuu Bara upo mikononi mwa Simba ambayo ilitwaa msimu uliopita, kwa sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 11. 

SOMA NA HII  KAGERE ATAJA KINACHOMBEBA NDANI YA SIMBA