Home news BAADA YA KUIFANYA SIMBA ISHINDWE KUPATA MATOKEO..MUGALU HUYOOO MBIONI …

BAADA YA KUIFANYA SIMBA ISHINDWE KUPATA MATOKEO..MUGALU HUYOOO MBIONI …


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Simba Mkongomani Chris Mugalu amepata nafuu ya majeraha yake na wiki hii huenda akaanza mazoezi ya binafsi ya timu. Hiyo ni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu baada ya kupata maumivu ya misuli hivi karibuni.

Mugalu hadi hivi sasa amekosa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana.

Akizungumza na Soka la Bongo, Daktari Mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe alisema kuwa mshambuliaji huyo anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu haraka.

Gembe alisema kuwa mshambuliaji huyo baada ya kupata nafuu huenda akaanza mazoezi wiki hii huku akiwa chini ya uangalizi.

“Wachezaji wetu Lwanga (Taddeo) Sakho (Ousmane), ndiyo wachezaji ambao bado hawapo fiti kwa asilimia mia moja kutokana na ukubwa wa majeraha yao waliyoyapata.

“Lakini Mugalu yeye amepata nafuu ya maumivu yake na huenda akawa sehemu ya wachezaji watakaotumika katika michezo ijayo,”alisema Gembe.

SOMA NA HII  A-Z JINSI SIMBA JANA ILIVYOITIBUA MIPANGO YA WANIGER...MORRISON AWA GUMZO...ATUMA SALAMU HUKU...