Home Uncategorized POLISI TANZANIA: KAZI BADO IPO KWENYE LIGI

POLISI TANZANIA: KAZI BADO IPO KWENYE LIGI

UONGOZI wa Polisi Tanzania umesema kuwa bado una kazi kubwa ya kufanya ndani ya Ligi Kuu ili kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.
Polisi Tanzania ipo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini aliyechukua mikoba ya Seleman Matola ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Simba akiwa ni Kocha Msaidizi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa mpango mkubwa wa timu yao ni kupata matokeo chanya yatakayowafanya wawe kwenye nafasi nzuri.
“Bado kwa sasa kikosi kinapambana kupata matokeo chanya, mipango ni mingi na kila kitu kipo sawa kikubwa ni kuona tunapata matokeo chanya yatakayotufanya tumalize ligi tukiwa kwenye nafasi nzuri,” amesema.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita kwenye ligi ikiwa na pointi 32 imecheza mechi 28 imebakiwa na mechi 10 kumaliza mzunguko wa pili.
SOMA NA HII  LUIS MIQUSSONE WA SIMBA NA CARLINHOS WAINGIA KWENYE VITA MPYA