Home Uncategorized Amunike kujaribu wengine leo

Amunike kujaribu wengine leo

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” leo inashuka dimbani kucheza mchezo wa pili wa Kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

Mchezo huo utakaochezwa saa 2 Usiku kwenye Uwanja wa El Sekka El Hadid,Cairo ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kuelekea kwenye mashindano ya AFCON yatakayoanza Juni 21,2019.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amesema atautumia mchezo huo kuwatazama wachezaji wengine ambao hawakutumika kwenye mchezo uliopita wa Kirafiki dhidi ya Misri ambao Tanzania ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Borg El Harab,Alexandria.

Amesema atawapumzisha baadhi ya Wachezaji ili kuwatazama pia wachezaji wengine.

Ameongeza kua mchezo dhidi ya Misri umesaidia kutoa picha ya namna mashindano ya AFCON yatakavyokuwa.

Tanzania ipo Kundi moja na Algeria,Senegal na Kenya na itaanza kibarua chake kwa kukipiga na Senegal Juni 23,2019.

The post Amunike kujaribu wengine leo appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  MZUNGU WA YANGA AWABADILISHIA MBINU WAPINZANI WAKE ADAI WACHEZAJI WAKE WAMECHOKA