Home Uncategorized SIMBA YACHANGIA YANGA KUPOTEZA MBELE YA KMC NAMNA HII

SIMBA YACHANGIA YANGA KUPOTEZA MBELE YA KMC NAMNA HII

PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa walitumia nguvu nyingi kupambana na Simba jambo lililowafanya washindwe kusepa na pointi tatu mbele ya KMC.

Yanga jana Machi 12 ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda Machi 8 Uwanja wa Taifa bao 1-0 mbele ya Simba.

Tshishimbi amesema kuwa walijipanga kusepa na pointi tatu mbele ya KMC ila bahati haikuwa yao kutokana na kutumia nguvu nyingi kwenye mechi ya dabi dhidi ya Simba.

“Tulitumia nguvu nyingi kwenye mechi ya dabi jambo ambalo limetufanya tushindwe kufanya vema mbele ya KMC, kupoteza kwetu sio mwisho wa mapambano kazi bado inaendelea,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 26 bao pekee la ushindi lilifungwa na Salim Aiyee dk ya 62. 

SOMA NA HII  ARSENAL YAMALIZANA NA MABEKI DAKIKA ZA USIKU, MENEJA AMPA TANO LUIZ