Home Habari za michezo FT: NAMUNGO 2-2 SIMBA ….’PAPATU PAPATU’ ZA KIBU DENIS LEO ZAONEKANA KUWA...

FT: NAMUNGO 2-2 SIMBA ….’PAPATU PAPATU’ ZA KIBU DENIS LEO ZAONEKANA KUWA NA UMUHIMU…


KIKOSI cha Namungo leo Mei 3,2022 kimeibana mbavu Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kupata sare ya kufungana mabao 2-2.

Ngoma imechezwa Uwanja wa Ilulu ambapo Namungo walianza kwa kasi kubwa kusaka ushindi na waliwatangulia Simba.

Ilikuwa dk ya 7 kupitia kwa Jacob Masawe aliyepachika bao hilo kwa kichwa kisha likawekwa usawa na Shomari kapombe.

Ngoma ilikuwa nzito ambapo Namungo walimtungua tena Aishi Manula dk ya 57 kupitia kwa Obrey Chirwa.

Mabingwa watetezi Simba waliendelea kupambana kwa mara nyingine tena na kusawazisha kupitia kwa Kiu Dennis.

Kapombe amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi ila wamekwama kupata kutokana na ushindani ambao ulikuwepo kwenye mchezo huo.

Ni Hashim Manyanya alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa Namungo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MANULA KUWA NNJE MSIMU MZIMA...UKWELI HALISI NI HUU HAPA...