Home Habari za michezo SHAFFIH DAUDA:- SIMBA WAMEKUBALI HAWANA TIMU BORA MSIMU HUU….

SHAFFIH DAUDA:- SIMBA WAMEKUBALI HAWANA TIMU BORA MSIMU HUU….

Habari za Simba leo

Timu ya Yanga imeendeleza ubabe dhidi ya Simba msimu huu baada ya kuitandika mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa jana Aprili 20, 2024 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Aziz Ki dakika ya 19′ kwa mkwaju wa penalti, bao la pili likifungwa na Joseph Guede dakika 39′ akimpiga chenga hadi kipa, Ayoub Lakred.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Mchambuzi wa masuala ya soka, Shaffih Dauda anasema; 1.NJE YA UWANJA Kwanza nimefurahi kuona kelele za mashabiki wa Simba sio nyingi kama ambavyo ilikuwa hapa kati kati, ni ishara kuwa tayari wamekubali kuwa hawana timu bora msimu huu.

Hii ni hatua ya kuanzia kwenye kujenga timu ini lazima kwanza ukubali hali ya timu yako, hakuna uongo woWote ambao mashabiki wa Simba wanataka kusikia kwa sasa.

Walishinikiza uongozi upishe lakini shinikizo halijazaa matunda, Viongozi waliopo kama wataendelea kuwepo wawatafutie furaha ya uhakika hawa mashabiki ambao kelele zao zinaqnzia kwa hao hao viongozi.

2.KIUFUNDI Simba SC imecheza michezo 21 ya Ligi kuu hadi sasa kati ya mechi 30, kimahesabu amebakisha mechi 9 ambazo ni sawa na alama 27 ,alama ambazo zinaweza kubadili chochote na kumfanya kuwa bingwa kama ambavyo viongozi wao wamekuwa wakiwaambia mashabiki wao.

Lakini kwa form ya Yanga ni nqumu hiko kutokea, Simba wakubali kuwa msimu umeisha kilichobaki ni kupigania nafasi ya pili ili washiriki Champions League msimu ujao.

Kwa upande wa wachezaji ni muda sasa wΔ… kila anayelipwΔ… na simba kuanza kupewa dakika ili kuona je 2024/25 ataendelea kuwepo au apishe nafasi wapewe wengine.

Wapo wachezaji wa kikosi cha kwanzq cha Simba hawashawishi kabisa kuwaangalia nafikiri hao hawana cha kubadilisha kwa mechi 9, Viongozi wafanye maamuzi magumu na wakifanya hivyo kile kikosi cha kwanza wanaweza kubaki sio zaidi ya wachezaji wanne.

SOMA NA HII  KISA MASHABIKI SIMBA JANA KUMPA 'WAZIMU'...MORRISON KAAMUA KUMTUNUKU MWANAE JINA JIPYA...