Home Uncategorized SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU HATMA YA LUIS NDANI YA KIKOSI HICHO

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU HATMA YA LUIS NDANI YA KIKOSI HICHO


UONGOZI wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 Simba umesema kuwa ,kiungo wao Luis Miquissone amezivutia timu nyingi nje ya nchi ambao wamekuwa wakiuliza kuhusu huduma ya nyota huyo.

Luis ambaye amebatizwa jina la Mmakonde amefunga jumla ya mabao matano kwenye ardhi ya Bongo katika mashindano yote ikiwa ni ndani ya ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ametupia mabao manne ndani ya ligi na pasi moja huku akiwa amefunga bao moja kwenye Kombe la Shirikisho, Julai 12 mbele ya Yanga.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amekuwa akiuliziwa na marafiki zake kutoka Ulaya ambao ni mawakala kuhusu kumpata nyota huyo.

“Rafiki zangu watatu ambao ni mawakala wakubwa Ulaya wameshaniulizia kuhusu huyu Mmakonde, na tajiri nishamwambia, but (lakini) Simba inahitaji Quality players (wachezaji bora) kama hawa ili kufanya vema katika Champions league msimu ujao.(Ligi ya Mabingwa Afrika).

SOMA NA HII  BALAA, KAGERE APEWA MABAO 30 LIGI KUU BARA