Home Habari za michezo WAKATI LEO NDIO LEO….MASTAA HAWA MUHIMU WA YANGA KUIKOSA SIMBA…NABI APAGAWA..

WAKATI LEO NDIO LEO….MASTAA HAWA MUHIMU WA YANGA KUIKOSA SIMBA…NABI APAGAWA..

KIUNGO mchetuaji wa Yanga, Bernard Morrison leo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Pia Crispin Ngushi huyu naye anatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho kwa kuwa hajawa fiti.

Sababu ya kukosekana kwenye mchezo huo ni kutokana na adhabu ambayo alipewa kutokana na kosa la kumkanyanga mchezaji wa Azam FC kwenye mchezo wa ligi walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wengine wapo tayari na mazoezi ya mwisho yataamua kikosi na wale ambao wataanza.

“Morrison atakosekana kwenye mchezo wetu  dhidi ya Simba kwa kuwa ana adhabu lakini wachezaji wengine wapo vizuri.

“Sure Boy yeye alikuwa anaumwa lakini amepona hivyo kuanza kwake pia itategemea mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba,” amesema Nabi.

SOMA NA HII  KISA UJIO WAKE SIMBA....CHAMA KUMTUPA NTIBAZONKIZA KWA SAKHO...ISHU IKO HIVI...