Home Habari za michezo KISA UJIO WAKE SIMBA….CHAMA KUMTUPA NTIBAZONKIZA KWA SAKHO…ISHU IKO HIVI…

KISA UJIO WAKE SIMBA….CHAMA KUMTUPA NTIBAZONKIZA KWA SAKHO…ISHU IKO HIVI…

Endapo Simba ikifanikisha kuinasa saini ya staa mwenye CV yake, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kuna mapro ambao kivyovyote watakula panga kulingana na kiwango wanachokionyesha ndani ya timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.

Watanzania waliona kiwango cha Saido kwa mara ya kwanza akicheza Yanga na msimu wa mwisho akiondoka aliacha rekodi ya mabao saba na asisti tatu, kisha akaibukia Geita Gold msimu huu ambako ana asisti sita na mabao manne.

Kitakwimu anatajwa kati ya wachezaji ambao wamefanya vizuri kwenye ligi hadi sasa ikiwa jana ulihitimishwa mzunguko wake wa kwanza.

Namba anayocheza Saido mara nyingi ndani ya Simba yupo mwamba wa Lusaka, Clatous Chama ambaye hawezi kuwekwa benchi kwani hadi sasa ana asisti saba na mabao mawili, ila wengine ni Pape Sakho (mabao matatu) na Agustine Okrah (mabao 3) ambao wanacheza pembeni, hao wanaweza wakawa kwenye mstari mwekundu wa kukaa benchi ama kukatwa ili kumpisha staa huyo raia wa Burundi.

Iko hivi; Simba ina kiungo mchezeshaji Chama ambaye anacheza nafasi moja na Saido lakini ni ngumu kwa Mzambia huyo kutoka kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ubora wake na mchango aliouonyesha ndani ya timu hiyo lakini ndiye kipenzi cha mashabiki.

Chama ambaye amecheza mechi 12, kati ya 15 za mzunguko wa kwanza amefunga mabao mawili, huku akitoa asisti saba na jumla amehusika kwenye mabao 9 kati ya 31 yaliyofungwa na timu yake.

Wakati Saido ambaye anaitumikia Geita Gold kwa sasa amefunga mabao manne na kutoa asisti sita jumla amehusika kwenye mabao 10 kati ya 17 yaliyofungwa na timu yake.

Hivyo namba zinampa nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza ukilinganisha na mawinga wawili ambao wamekuwa wakipewa nafasi ya kucheza na Okrah Sakho au wakati mwingine kwenye nafasi hii amekuwa akicheza Kibu Denis.

Simba ambayo ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda imeimarika nafasi zote isipokuwa winga wa kulia ambayo haina mchezaji ambaye ni chaguo la kwanza kikosi cha kwanza.

Mgunda amefanikiwa kutengeneza pacha nzuri ya beki wa na mara kwa mara pembeni wamekuwa wakicheza Mohammed Hussein Tshabalala na Shomary Kapombe, kati Henock Inonga na Joash Onyango huku eneo la kiungo mkabaji akimtumia zaidi Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin na kumi Chama, tisa Moses Phiri lakini eneo la winga halina chaguo kutokana na wachezaji kubadilika badilika.

WADAU WATOA NENO

Kocha Abdul Mingange, alisema bado Saido ni mchezaji mzuri akiendeleza juhudi zake ana nafasi nzuri ya kurudi katika timu kubwa kutokana na uzoefu alionao na ana kipaji kikubwa. Upande wa kuongeza nguvu Simba ambayo tayari ina Chama ni jambo zuri litaongeza changamoto, alisema.

“Simba wana Chama lakini hawana mtu mwingine anayeweza kucheza ikitokea huyo wanayemtegemea kaumia. Pia Saido anaweza kucheza sambamba na Chama na wakaitengenezea timu matokeo mazuri kwa sababu wote wanaweza kufunga na kutengeneza nafasi.”

SOMA NA HII  FT: TANZANIA PRISONS 1-0 SIMBA SC...KISASI CHALIPWA SOKOINE...JAHAZI LA SIMBA LAZIDI KUTITIA MIKOANI...