Home epl GUARDIOLA: KLOPP AMENIFANYA NIWE BORA

GUARDIOLA: KLOPP AMENIFANYA NIWE BORA


 KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kocha wa Liverpool, Jorgen Klopp amemfanya azidi kuwa kocha bora kutokana na changamoto anayompa nakumfanya kila siku awe anafikiria mbinu mpya za kushinda michezo, Pep amesema hayo baada ya kutumiwa ujumbe wa pongezi na kocha huyo.

 

Baada ya City kutwaa ubingwa wa EPL Kocha wa Liverpool, Jorgen Klopp ambaye pia alikuwa mshindani wa Pep Guardiola nchini Ujerumani wakati Klopp akiwa na kikosi cha Dortmund na Pep akiwa na kikosi cha Bayern Munich, amemtumia ujumbe wa pongezi Goardiola kwa kumpongeza kwa mafanikio aliyoyapata msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

 

Baada ya kupokea salaam hizo za pongezi Pep raia wa Hispania amesema; “Ninathamini sana, yeye na meneja wa Everton Carlo Ancelotti wamefanya hivyo, kwa hivyo nathamini sana wote wawili. Bado sijapata nafasi ya kujibu ujumbe, lakini nitafanya leo.

 

“Jurgen, kwa kweli, ni msukumo mkubwa kwangu na amenifanya kuwa bora kupitia timu zake wakati yupo Borussia Dortmund na sasa Liverpool niwe meneja bora. Ananifanya nifikirie sana juu ya michezo ninayocheza na kila kitu.”

 

Manchester City walitangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu huu wa 2020-21 siku ya Jumanne baada ya Manchester United kufungwa mabao 2-1 na Leicester City, na kufanya tofauti ya alama kati ya Man City na majirani zao hao kuwa alamao 10 huku ikiwa imesalia michezo mitatu tu kabla ya Ligi kumalizika, hivyo alama 80 walizonazo City haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

 

Guardiola mwenye umri wa miaka 50 ameshinda jumla ya makombe nane (8) makubwa tangu ajiunge na Manchester City mwaka 2016 na bado ana nafasi ya kuongeza kombe jingine endapo kama atafanikiwa kuifunga Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Chelsea mchezo utakao chezwa Mei 29, 2021.

SOMA NA HII  HUYU HAPA MCHEZAJI WA KITANZANIA KUTOKA ZNZ ALIYEMLIZA MOURINHO JUZI..AFUNGUKA HAYA