Home kimataifa HUYU HAPA MCHEZAJI WA KITANZANIA KUTOKA ZNZ ALIYEMLIZA MOURINHO JUZI..AFUNGUKA HAYA

HUYU HAPA MCHEZAJI WA KITANZANIA KUTOKA ZNZ ALIYEMLIZA MOURINHO JUZI..AFUNGUKA HAYA


CHEZEA kipigo wewe!! Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho ilimbidi ageuke mbogo baada ya timu yake kukumbana na mvua ya mabao 6-1 kutoka kwa Bod¯ / Glimt anayoichezea Mzanzibar, Amahl Pellegrino kwenye Europa Conference Ligi.

AS Roma ilikumbana na kipigo hicho huko Norway na kuwaacha midomo wazi wadau mbalimbali wa soka la Ulaya kwani ni kitu ambacho hakikutegemewa.

Pellegrino alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walimuumiza Mourinho kwa kutupia bao moja dakika ya 78 baada ya kupewa asisti na Erik Botheim.

Mara baada ya mchezo huo, Mourinho alisema, “Tuna timu moja nzuri lakini hatuna kikosi bora, leo (siku hiyo) hatukucheza tukiwa kama timu, tulicheza kama kikosi tu na mwisho wa siku tumeadhibiwa.

“Siwezi kusema nitumie wachezaji wale wale kwenye kila mchezo, kwa kufanya hivyo nitawahatarisha, kuna tofauti kubwa ya wachezaji wa kikosi changu cha kwanza na wale ambao ni chaguo la pili. Nilitegemea makubwa kutoka kwao lakini ni jukumu langu hili kuhakikisha wanakuwa bora,” alisema kocha huyo.

Kwa upande wake, Pellegrino ambaye anatamani kuichezea Taifa Stars, alisema: “Haikuwa rahisi kuifunga AS Roma, “Ilitubidi kujitoa kuliko kawaida, tunaufahamu ubora wao.”

SOMA NA HII  CAVAN KUPEWA MKATABA MNONO UNITED